Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha Bwana akasema, “Mwite Lo-Ami* kwa maana ninyi si watu wangu, nami si Mungu wenu.

Hosea 1:9 in English

Hosea 1:9 · Berean Standard Bible

And the LORD said, “Name him Lo-ammi,* for you are not My people, and I am not your God.*

Context

7Hata hivyo nitaonyesha upendo kwa nyumba ya Yuda, nami nitawaokoa si kwa upinde, upanga au vita, wala kwa farasi na wapanda farasi, bali kwa njia ya Bwana Mungu wao.” 8Baada ya Gomeri kumwachisha Lo-Ruhama kunyonya, Gomeri alipata mwana mwingine. 9Kisha Bwana akasema, “Mwite Lo-Ami* kwa maana ninyi si watu wangu, nami si Mungu wenu. 10“Hata hivyo Waisraeli watakuwa kama mchanga kando ya bahari, ambao hauwezi kupimika wala kuhesabiwa. Mahali pale walipoambiwa, ‘Ninyi si watu wangu,’ wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’ 11Watu wa Yuda na watu wa Israeli wataunganishwa tena, nao watamchagua kiongozi mmoja nao watakwea watoke katika nchi, kwa kuwa siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.