Waebrania 5:4
Hebrews 5:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakuna anayejitwalia heshima hii mwenyewe; ni lazima aitwe na Mungu, kama vile Aroni alivyoitwa.
Hebrews 5:4 in English
Hebrews 5:4 · Berean Standard Bible
No one takes this honor upon himself; he must be called by God, just as Aaron was.
Context
2Kwa kuwa yeye mwenyewe ni dhaifu, aweza kuwachukulia kwa upole wale wasiojua na kupotoka. 3Hii ndiyo sababu inampasa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe na vivyo hivyo kwa ajili ya dhambi za watu. 4Hakuna anayejitwalia heshima hii mwenyewe; ni lazima aitwe na Mungu, kama vile Aroni alivyoitwa. 5Pia Kristo hakujitwalia utukufu yeye mwenyewe wa kuwa Kuhani Mkuu, bali Mungu alimwambia,
“Wewe ni Mwanangu;
leo mimi nimekuzaa.” 6Pia mahali pengine asema,
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.