Waebrania 1:4
Hebrews 1:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo alifanyika bora kuliko malaika, kama jina alilorithi lilivyo bora kuliko lao.
Hebrews 1:4 in English
Hebrews 1:4 · Berean Standard Bible
So He became as far superior to the angels as the name He has inherited is excellent beyond theirs.
Context
2lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu. 3Mwana ni mngʼao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni. 4Kwa hiyo alifanyika bora kuliko malaika, kama jina alilorithi lilivyo bora kuliko lao. 5Kwa maana ni malaika yupi ambaye wakati wowote Mungu alipata kumwambia,
“Wewe ni Mwanangu;
leo mimi nimekuzaa?”
Au tena,
“Mimi nitakuwa Baba yake,
naye atakuwa Mwanangu?” 6Tena, Mungu amletapo mzaliwa wake wa kwanza ulimwenguni, anasema,
“Malaika wote wa Mungu na wamsujudu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.