Habakuki 3:5
Habakkuk 3:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tauni ilimtangulia; maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake.
Habakkuk 3:5 in English
Habakkuk 3:5 · Berean Standard Bible
Plague went before Him, and fever followed in His steps.
Context
3Mungu alitoka Temani,
yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani.
Utukufu wake ulifunika mbingu,
na sifa zake zikaifunika dunia. 4Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo;
mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake,
ambako nguvu zake zilifichwa. 5Tauni ilimtangulia;
maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake. 6Alisimama, akaitikisa dunia;
alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke.
Milima ya zamani iligeuka mavumbi
na vilima vilivyozeeka vikaanguka.
Njia zake ni za milele. 7Niliona watu wa Kushani katika dhiki,
na makazi ya Midiani katika maumivu makali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.