Habakuki 2:17
Habakkuk 2:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika, na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha. Kwa sababu umemwaga damu ya mtu; umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliyeko ndani yake.
Habakkuk 2:17 in English
Habakkuk 2:17 · Berean Standard Bible
For your violence against Lebanon will overwhelm you, and the destruction of animals will terrify you, because of your bloodshed against men and your violence against the land, the city, and all their dwellers.
Context
15“Ole wake yeye awapaye jirani zake kileo,
akiimimina kutoka kwenye kiriba
cha mvinyo mpaka wamelewa,
ili apate kutazama miili yao iliyo uchi. 16Utajazwa na aibu badala ya utukufu.
Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue!
Kikombe kutoka kwenye mkono wa kuume wa Bwana kinakujia,
na aibu itafunika utukufu wako. 17Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika,
na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha.
Kwa sababu umemwaga damu ya mtu;
umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliyeko ndani yake. 18“Sanamu ina thamani gani,
kwani mwanadamu ndiye alichonga?
Ama kinyago kinachofundisha uongo?
Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza
hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe;
hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza. 19Ole wake yeye auambiaye mti, ‘Uwe hai!’
Ama asemaye na jiwe lisilo na uhai, ‘Amka!’
Je, linaweza kuongoza?
Limefunikwa kwa dhahabu na fedha;
hakuna pumzi ndani yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.