Native Bible

Habakkuk 1:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ee Bwana, hata lini nitakuomba msaada, lakini wewe husikilizi? Au kukulilia, “Udhalimu!” Lakini hutaki kuokoa?

Habakkuk 1:2 in English

Habakkuk 1:2 · Berean Standard Bible

How long, O LORD, must I call for help but You do not hear, or cry out to You, “Violence!” but You do not save?

Context

1Neno alilopokea nabii Habakuki. 2Ee Bwana, hata lini nitakuomba msaada, lakini wewe husikilizi? Au kukulilia, “Udhalimu!” Lakini hutaki kuokoa? 3Kwa nini unanifanya nitazame dhuluma? Kwa nini unavumilia makosa? Uharibifu na udhalimu viko mbele yangu; kuna mabishano na mapambano kwa wingi. 4Kwa hiyo sheria imepotoshwa, nayo haki haipo kabisa. Waovu wanawazunguka wenye haki, kwa hiyo haki imepotoshwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.