Native Bible

Genesis 9:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani.

Genesis 9:10 in English

Genesis 9:10 · Berean Standard Bible

and with every living creature that was with you—the birds, the livestock, and every beast of the earth—every living thing that came out of the ark.

Context

8Ndipo Mungu akamwambia Noa na wanawe pamoja naye: 9“Sasa mimi ninaweka Agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu, 10pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani. 11Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.” 12Mungu akasema, “Hii ni ishara ya Agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, Agano kwa vizazi vyote vijavyo:

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.