Native Bible

Genesis 7:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji.

Genesis 7:18 in English

Genesis 7:18 · Berean Standard Bible

So the waters continued to surge and rise greatly on the earth, and the ark floated on the surface of the waters.

Context

16Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Noa, ndipo Bwana akamfungia ndani. 17Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi. 18Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji. 19Maji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote. 20Maji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano.*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.