Mwanzo 5:3
Genesis 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi.
Genesis 5:3 in English
Genesis 5:3 · Berean Standard Bible
When Adam was 130 years old, he had a son in his own likeness, after his own image; and he named him Seth.
Context
1Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu.
Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. 2Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.” 3Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi. 4Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 5Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.