Mwanzo 48:8
Genesis 48:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati Israeli alipowaona wana wa Yosefu, akauliza, “Hawa ni nani?”
Genesis 48:8 in English
Genesis 48:8 · Berean Standard Bible
When Israel saw the sons of Joseph, he asked, “Who are these?”
Context
6Lakini watoto utakaowazaa baada yao watakuwa wako. Katika nchi watakayoirithi, watatambuliwa kwa jina la ndugu zao. 7Nilipokuwa ninarudi kutoka Padani, katika huzuni yangu Raheli alifariki katika nchi ya Kanaani tulipokuwa tungali tukisafiri, tukiwa karibu kufika Efrathi. Kwa hiyo nilimzika huko, kando ya njia iendayo Efrathi” (yaani Bethlehemu). 8Wakati Israeli alipowaona wana wa Yosefu, akauliza, “Hawa ni nani?” 9Yosefu akamjibu baba yake, “Hawa ni wana ambao Mungu amenipa nikiwa huku.”
Ndipo Israeli akasema, “Walete kwangu ili niwabariki.” 10Basi macho ya Israeli yalikuwa hayaoni vizuri kwa sababu ya uzee, naye aliona kwa shida. Kwa hiyo Yosefu akawaleta wanawe karibu na baba yake, Israeli akawabusu na akawakumbatia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.