Mwanzo 48:3
Genesis 48:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yakobo akamwambia Yosefu, “Mungu Mwenyezi* alinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani, huko akanibariki,
Genesis 48:3 in English
Genesis 48:3 · Berean Standard Bible
Jacob said to Joseph, “God Almighty * appeared to me at Luz in the land of Canaan, and there He blessed me
Context
1Baada ya muda Yosefu akaambiwa kwamba, “Baba yako ni mgonjwa.” Kwa hiyo akawachukua wanawe wawili Manase na Efraimu, pamoja naye. 2Yakobo alipoambiwa, “Mwanao Yosefu amekujia kukuona,” Israeli akakusanya nguvu zake, akaketi kitandani. 3Yakobo akamwambia Yosefu, “Mungu Mwenyezi* alinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani, huko akanibariki, 4naye akaniambia, ‘Nitakufanya ustawi na kuongezeka hesabu yako, nitakufanya kuwa jamii ya mataifa, nami nitakupa nchi hii uimiliki milele wewe na wazao wako baada yako.’ 5“Sasa basi, wanao wawili waliozaliwa kwako huku Misri kabla sijaja hapa kwako watahesabiwa kuwa ni wangu; Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama vile Reubeni na Simeoni walivyo wangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.