Mwanzo 48:11
Genesis 48:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Israeli akamwambia Yosefu, “Kamwe sikutazamia kuuona uso wako tena, lakini sasa Mungu ameniruhusu kuwaona watoto wako pia.”
Genesis 48:11 in English
Genesis 48:11 · Berean Standard Bible
“I never expected to see your face again,” Israel said to Joseph, “but now God has let me see your children as well.”
Context
9Yosefu akamjibu baba yake, “Hawa ni wana ambao Mungu amenipa nikiwa huku.”
Ndipo Israeli akasema, “Walete kwangu ili niwabariki.” 10Basi macho ya Israeli yalikuwa hayaoni vizuri kwa sababu ya uzee, naye aliona kwa shida. Kwa hiyo Yosefu akawaleta wanawe karibu na baba yake, Israeli akawabusu na akawakumbatia. 11Israeli akamwambia Yosefu, “Kamwe sikutazamia kuuona uso wako tena, lakini sasa Mungu ameniruhusu kuwaona watoto wako pia.” 12Ndipo Yosefu akawaondoa wanawe magotini mwa Israeli naye akasujudu hadi nchi. 13Yosefu akachukua wale wana wawili, Efraimu kwenye mkono wake wa kuume akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kushoto akimwelekeza kwenye mkono wa kuume wa Israeli, akawaleta karibu na babu yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.