Mwanzo 46:7
Genesis 46:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote mpaka Misri.
Genesis 46:7 in English
Genesis 46:7 · Berean Standard Bible
Jacob took with him to Egypt his sons and grandsons, and his daughters and granddaughters—all his offspring.
Context
5Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao aliyokuwa amempelekea kumsafirisha. 6Wakachukua pia mifugo yao na mali walizokuwa wamezipata Kanaani, Yakobo na uzao wake wote wakashuka Misri. 7Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote mpaka Misri. 8Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri:
Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. 9Wana wa Reubeni ni:
Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.