Mwanzo 36:7
Genesis 36:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao.
Genesis 36:7 in English
Genesis 36:7 · Berean Standard Bible
For their possessions were too great for them to dwell together; the land where they stayed could not support them because of their livestock.
Context
5Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani. 6Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake. 7Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao. 8Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya kilima huko Seiri. 9Hawa ndio wazao wa Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya kilima cha Seiri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.