Native Bible

Genesis 32:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ngamia wake thelathini pamoja na ndama zao, ngʼombe wake arobaini na mafahali kumi, punda wake ishirini na punda waume kumi.

Genesis 32:15 in English

Genesis 32:15 · Berean Standard Bible

30 milk camels with their young, 40 cows, 10 bulls, 20 female donkeys, and 10 male donkeys.

Context

13Akalala pale usiku ule, miongoni mwa vitu alivyokuwa navyo, akachagua zawadi kwa ajili ya Esau ndugu yake: 14Mbuzi waume ishirini na mbuzi wake 200, kondoo dume ishirini na kondoo wake 200. 15Ngamia wake thelathini pamoja na ndama zao, ngʼombe wake arobaini na mafahali kumi, punda wake ishirini na punda waume kumi. 16Akaviweka chini ya uangalizi wa watumishi wake, kila kundi peke yake na kuwaambia, “Nitangulieni na kuacha nafasi kati ya makundi.” 17Akamwagiza yule aliyetangulia kuwa, “Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, ‘Wewe ni wa nani? Unakwenda wapi? Wanyama hawa wote mbele yako ni mali ya nani?’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.