Mwanzo 3:9
Genesis 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?”
Genesis 3:9 in English
Genesis 3:9 · Berean Standard Bible
But the LORD God called out to the man, “Where are you?”
Context
7Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika. 8Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani. 9Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?” 10Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.” 11Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.