Mwanzo 29:12
Genesis 29:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yakobo alikuwa amemwambia Raheli kuwa yeye alikuwa jamaa ya baba yake, na kwamba ni mwana wa Rebeka. Basi Raheli alikimbia na kumweleza baba yake.
Genesis 29:12 in English
Genesis 29:12 · Berean Standard Bible
He told Rachel that he was Rebekah’s son, a relative of her father, and she ran and told her father.
Context
10Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mama yake, pamoja na kondoo wa Labani, alikwenda na kulivingirisha jiwe kutoka mdomoni mwa kisima na kuwanywesha kondoo wa mjomba wake. 11Kisha Yakobo akambusu Raheli na akaanza kulia kwa sauti. 12Yakobo alikuwa amemwambia Raheli kuwa yeye alikuwa jamaa ya baba yake, na kwamba ni mwana wa Rebeka. Basi Raheli alikimbia na kumweleza baba yake. 13Mara Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo, mwana wa ndugu yake, aliharakisha kwenda kumlaki. Akamkumbatia na kumbusu, halafu akamleta nyumbani kwake, kisha Yakobo akamwambia mambo yote. 14Ndipo Labani akamwambia, “Wewe ni nyama yangu na damu yangu mwenyewe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.