Native Bible

Genesis 28:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mungu Mwenyezi* na akubariki uwe na uzao uongezeke idadi yako upate kuwa jamii kubwa ya watu.

Genesis 28:3 in English

Genesis 28:3 · Berean Standard Bible

May God Almighty * bless you and make you fruitful and multiply you, so that you may become a company of peoples.

Context

1Basi Isaki akamwita Yakobo, akambariki na akamwamuru, akisema, “Usioe mwanamke wa Kikanaani. 2Nenda mara moja mpaka Padan-Aramu, kwenye nyumba ya Bethueli baba wa mama yako. Uchukue mke kati ya binti za Labani ambaye ni ndugu wa mama yako. 3Mungu Mwenyezi* na akubariki uwe na uzao uongezeke idadi yako upate kuwa jamii kubwa ya watu. 4Na akupe wewe na uzao wako baraka aliyopewa Abrahamu, upate kumiliki nchi unayoishi sasa kama mgeni, nchi ambayo Mungu alimpa Abrahamu.” 5Kisha Isaki akamuaga Yakobo, naye akaenda Padan-Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, ndugu wa Rebeka, aliyekuwa mama wa Yakobo na Esau.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.