Native Bible

Genesis 28:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nenda mara moja mpaka Padan-Aramu, kwenye nyumba ya Bethueli baba wa mama yako. Uchukue mke kati ya binti za Labani ambaye ni ndugu wa mama yako.

Genesis 28:2 in English

Genesis 28:2 · Berean Standard Bible

“Go at once to Paddan-aram,* to the house of your mother’s father Bethuel, and take a wife from among the daughters of Laban, your mother’s brother.

Context

1Basi Isaki akamwita Yakobo, akambariki na akamwamuru, akisema, “Usioe mwanamke wa Kikanaani. 2Nenda mara moja mpaka Padan-Aramu, kwenye nyumba ya Bethueli baba wa mama yako. Uchukue mke kati ya binti za Labani ambaye ni ndugu wa mama yako. 3Mungu Mwenyezi* na akubariki uwe na uzao uongezeke idadi yako upate kuwa jamii kubwa ya watu. 4Na akupe wewe na uzao wako baraka aliyopewa Abrahamu, upate kumiliki nchi unayoishi sasa kama mgeni, nchi ambayo Mungu alimpa Abrahamu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.