Native Bible

Genesis 27:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Uniandalie aina ya chakula kitamu nikipendacho uniletee nile, ili niweze kukubariki kabla sijafa.”

Genesis 27:4 in English

Genesis 27:4 · Berean Standard Bible

Then prepare a tasty dish that I love and bring it to me to eat, so that I may bless you before I die.”

Context

2Isaki akasema, “Mimi sasa ni mzee na sijui siku ya kifo changu. 3Sasa basi, chukua silaha zako, podo na upinde, uende nyikani, ukawinde nyama pori kwa ajili yangu. 4Uniandalie aina ya chakula kitamu nikipendacho uniletee nile, ili niweze kukubariki kabla sijafa.” 5Basi Rebeka alikuwa akisikiliza Isaki alipokuwa akizungumza na mwanawe Esau. Esau alipoondoka kwenda nyikani kuwinda nyama pori na kuleta, 6Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, “Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.