Mwanzo 27:30
Genesis 27:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada ya Isaki kumaliza kumbariki na baada tu ya Yakobo kuondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni.
Genesis 27:30 in English
Genesis 27:30 · Berean Standard Bible
As soon as Isaac had finished blessing him and Jacob had left his father’s presence, his brother Esau returned from the hunt.
Context
28Mungu na akupe umande kutoka mbinguni
na utajiri wa duniani:
wingi wa nafaka na divai mpya. 29Mataifa na yakutumikie
na mataifa yakusujudie.
Uwe bwana juu ya ndugu zako,
na wana wa mama yako wakusujudie.
Walaaniwe wale wakulaanio,
nao wale wakubarikio wabarikiwe.” 30Baada ya Isaki kumaliza kumbariki na baada tu ya Yakobo kuondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni. 31Naye pia akaandaa chakula kitamu akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.” 32Isaki baba yake akamuuliza, “Wewe ni nani?”
Akajibu, “Mimi ni mwanao, mzaliwa wako wa kwanza, Esau.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.