Native Bible

Genesis 26:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi Isaki akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa.

Genesis 26:30 in English

Genesis 26:30 · Berean Standard Bible

So Isaac prepared a feast for them, and they ate and drank.

Context

28Wakamjibu, “Tuliona wazi kuwa Bwana alikuwa pamoja nawe, kwa hiyo tukasema, ‘Inabidi kuwe na kiapo cha mapatano kati yetu, kati yetu na wewe. Na tufanye mkataba pamoja nawe 29kwamba hutatudhuru, kama jinsi nasi hatukuwanyanyasa bali tuliwatendea mema wakati wote na kuwaondoa kwetu kwa amani. Tena sasa umebarikiwa na Bwana.’ ” 30Basi Isaki akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa. 31Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaki akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaki kwa amani. 32Siku hiyo watumishi wa Isaki wakaja wakampa habari kuhusu kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, “Tumepata maji!”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.