Mwanzo 24:59
Genesis 24:59 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo wakamwaga ndugu yao Rebeka aondoke, pamoja na mjakazi wake, mtumishi wa Abrahamu na watu wake.
Genesis 24:59 in English
Genesis 24:59 · Berean Standard Bible
So they sent their sister Rebekah on her way, along with her nurse and Abraham’s servant and his men.
Context
57Ndipo wakasema, “Acha tumwite huyo binti tumuulize, tusikie atakavyosema.” 58Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, “Je, utakwenda na mtu huyu?”
Akasema, “Nitakwenda.” 59Hivyo wakamwaga ndugu yao Rebeka aondoke, pamoja na mjakazi wake, mtumishi wa Abrahamu na watu wake. 60Wakambariki Rebeka, wakamwambia,
“Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu,
mara elfu nyingi,
nao wazao wako wamiliki
malango ya adui zao.” 61Rebeka na vijakazi wake wakajiandaa, wakapanda ngamia zao wakafuatana na yule mtu. Hivyo yule mtumishi akamchukua Rebeka akaondoka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.