Mwanzo 24:28
Genesis 24:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yule msichana akakimbia akawaeleza watu wa nyumbani mwa mama yake kuhusu mambo haya.
Genesis 24:28 in English
Genesis 24:28 · Berean Standard Bible
The girl ran and told her mother’s household about these things.
Context
26Yule mtumishi akasujudu na kumwabudu Bwana, 27akisema, “Atukuzwe Bwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuondoa wema na uaminifu wake kwa bwana wangu. Mimi nami, Bwana ameniongoza safarini akanifikisha nyumbani kwa jamaa za bwana wangu.” 28Yule msichana akakimbia akawaeleza watu wa nyumbani mwa mama yake kuhusu mambo haya. 29Rebeka alikuwa na kaka aliyeitwa Labani, huyo akaharakisha kukutana na yule mtumishi kule kisimani. 30Mara alipoiona ile pete puani, na bangili mikononi mwa dada yake na kusikia yale maneno Rebeka aliyoambiwa na huyo mtumishi, alimwendea huyo mtumishi, akamkuta amesimama karibu na ngamia wake pale karibu na kisima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.