Mwanzo 21:19
Genesis 21:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.
Genesis 21:19 in English
Genesis 21:19 · Berean Standard Bible
Then God opened her eyes, and she saw a well of water. So she went and filled the skin with water and gave the boy a drink.
Context
17Mungu akamsikia kijana akilia, malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni na kumwambia, “Kuna nini Hagari? Usiogope, Mungu amesikia kijana analia akiwa amelala pale. 18Mwinue kijana na umshike mkono, kwa maana nitamfanya kuwa taifa kubwa.” 19Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe. 20Mungu akawa pamoja na huyu kijana alipokuwa akiendelea kukua. Aliishi jangwani na akawa mpiga upinde. 21Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akampatia mke kutoka Misri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.