Native Bible

Genesis 20:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?”

Genesis 20:10 in English

Genesis 20:10 · Berean Standard Bible

Abimelech also asked Abraham, “What prompted you to do such a thing?”

Context

8Kesho yake asubuhi na mapema Abimeleki akawaita maafisa wake wote, na baada ya kuwaambia yote yaliyotokea, waliogopa sana. 9Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu na kumwambia, “Wewe umetufanyia nini? Nimekukosea nini hata ukaleta hatia kubwa namna hii juu yangu na ufalme wangu? Umenifanyia mambo ambayo hayakupasa kufanyika.” 10Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?” 11Abrahamu akajibu, “Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ 12Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.