Mwanzo 2:4
Genesis 2:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa. Bwana Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
Genesis 2:4 in English
Genesis 2:4 · Berean Standard Bible
This is the account of the heavens and the earth when they were created, in the day that the LORD * God made them.
Context
2Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. 3Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya. 4Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa.
Bwana Mungu alipoziumba mbingu na dunia, 5hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi, 6lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.