Mwanzo 18:3
Genesis 18:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako.
Genesis 18:3 in English
Genesis 18:3 · Berean Standard Bible
“My lord,” said Abraham, “if I have found favor in your sight, please do not pass your servant by.
Context
1Bwana akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. 2Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi. 3Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako. 4Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu. 5Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.”
Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.