Mwanzo 18:17
Genesis 18:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Bwana akasema, “Je, nimfiche Abrahamu jambo ninalokusudia kufanya?
Genesis 18:17 in English
Genesis 18:17 · Berean Standard Bible
And the LORD said, “Shall I hide from Abraham what I am about to do?
Context
15Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.”
Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!” 16Wakati watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, Abrahamu akawatoa kitambo kidogo ili awasindikize. 17Ndipo Bwana akasema, “Je, nimfiche Abrahamu jambo ninalokusudia kufanya? 18Hakika Abrahamu atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, kupitia kwake mataifa yote ya dunia yatabarikiwa. 19Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya Bwana, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili Bwana atimize ahadi yake kwa Abrahamu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.