Mwanzo 18:11
Genesis 18:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Abrahamu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
Genesis 18:11 in English
Genesis 18:11 · Berean Standard Bible
And Abraham and Sarah were already old and well along in years; Sarah had passed the age of childbearing.
Context
9Wakamuuliza, “Yuko wapi Sara mkeo?”
Akasema, “Yuko huko, ndani ya hema.” 10Kisha Bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.”
Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake. 11Abrahamu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 12Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?” 13Ndipo Bwana akamwambia Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.