Native Bible

Galatians 3:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi mpatanishi huhusisha zaidi ya upande mmoja, lakini Mungu ni mmoja.

Galatians 3:20 in English

Galatians 3:20 · Berean Standard Bible

A mediator is unnecessary, however, for only one party; but God is one.

Context

18Kwa maana kama urithi hupatikana kwa sheria, basi hautegemei tena ahadi, lakini Mungu kwa neema yake alimpa Abrahamu urithi kwa njia ya ahadi. 19Kwa nini basi iwepo sheria? Sheria iliwekwa kwa sababu ya makosa mpaka atakapokuja yule Mzao wa Abrahamu, ambaye alitajwa katika ile ahadi. Sheria iliamriwa na malaika kwa mkono wa mpatanishi. 20Basi mpatanishi huhusisha zaidi ya upande mmoja, lakini Mungu ni mmoja. 21Je basi, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa maana kama sheria iliyotolewa ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki ingepatikana kwa njia ya sheria. 22Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo yapate kupewa wale wanaoamini.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.