Ezra 5:9
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tuliwauliza viongozi, “Ni nani aliyewapa ruhusa kujenga upya Hekalu hili na kurejeza hali ya jengo kama lilivyokuwa?”
Ezra 5:9 in English
Ezra 5:9 · Berean Standard Bible
So we questioned the elders and asked, “Who authorized you to rebuild this temple and restore this structure?”
Context
7Taarifa waliyompelekea ilisomeka kama ifuatavyo:
Kwa Mfalme Dario:
Salamu kwa moyo mkunjufu. 8Inampasa Mfalme ajue kwamba tulikwenda katika eneo la Yuda, kwenye Hekalu la Mungu mkuu. Watu wanalijenga kwa mawe makubwa na kuweka mbao kwenye kuta. Kazi inafanyika kwa bidii na inaendelea kwa haraka chini ya uongozi wao. 9Tuliwauliza viongozi, “Ni nani aliyewapa ruhusa kujenga upya Hekalu hili na kurejeza hali ya jengo kama lilivyokuwa?” 10Pia tuliwauliza majina yao, ili tukuandikie kukujulisha majina ya viongozi wao. 11Hili ndilo jibu walilotupa:
“Sisi ni watumishi wa Mungu wa mbingu na nchi, nasi tunalijenga upya Hekalu ambalo lilijengwa miaka mingi iliyopita, lile ambalo mfalme mkuu wa Israeli alilijenga na kulikamilisha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.