Ezekieli 7:25
Ezekiel 7:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hofu ya ghafula itakapokuja, watatafuta amani, lakini haitakuwepo.
Ezekiel 7:25 in English
Ezekiel 7:25 · Berean Standard Bible
Anguish is coming! They will seek peace, but find none.
Context
23“Andaa minyororo, kwa sababu nchi imejaa umwagaji wa damu na mji umejaa udhalimu. 24Nitaleta taifa ovu kuliko yote ili kumiliki nyumba zao, nitakomesha kiburi cha wenye nguvu na mahali pao patakatifu patatiwa unajisi. 25Hofu ya ghafula itakapokuja, watatafuta amani, lakini haitakuwepo. 26Maafa juu ya maafa yatakuja, tetesi ya mabaya juu ya tetesi ya mabaya. Watajitahidi kupata maono kutoka kwa nabii, mafundisho ya sheria toka kwa kuhani yatapotea, vivyo hivyo shauri kutoka kwa wazee. 27Mfalme ataomboleza, mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa, nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka. Nitawashughulikia sawasawa na matendo yao na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu. Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi Bwana.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.