Native Bible

Ezekiel 45:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Katika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000.* Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, Patakatifu pa Patakatifu.

Ezekiel 45:3 in English

Ezekiel 45:3 · Berean Standard Bible

From this holy portion, you are to measure off a length of 25,000 cubits and a width of 10,000 cubits,* and in it will be the sanctuary, the Most Holy Place.*

Context

1“ ‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwa Bwana kuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa 25,000,* upana wake dhiraa 20,000* eneo hili lote litakuwa takatifu. 2Katika hiyo, itakuwepo sehemu mraba ambayo ni mahali patakatifu kila upande dhiraa 500 ikiwa imezungukwa na eneo la wazi lenye upana wa dhiraa hamsini. 3Katika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000.* Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, Patakatifu pa Patakatifu. 4Itakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za Bwana. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu. 5Eneo la urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000 litakuwa la Walawi wale wanaotumika hekaluni, kama milki yao kwa ajili ya miji ya kuishi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.