Ezekieli 45:10
Ezekiel 45:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tumieni mizani sahihi na vipimo sahihi vya efa* na bathi.*
Ezekiel 45:10 in English
Ezekiel 45:10 · Berean Standard Bible
You must use honest scales, a just ephah,* and a just bath.*
Context
8Nchi hii itakuwa milki yake katika Israeli. Nao wakuu wangu hawataonea tena watu wangu bali watairuhusu nyumba ya Israeli kuimiliki nchi kulingana na makabila yao. 9“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Yatosha, enyi wakuu wa Israeli! Acheni mbali ukatili wenu na uonevu wenu mkafanye lile lililo haki na sawa. Acheni kuwatoza watu wangu isivyo haki, asema Bwana Mwenyezi. 10Tumieni mizani sahihi na vipimo sahihi vya efa* na bathi.* 11Efa na bathi viwe sawa, bathi iwe sehemu ya kumi ya homeri na efa iwe sehemu ya kumi ya homeri, homeri itakuwa ndicho kiwango cha kukubalika kwa vyote viwili. 12Shekeli moja itakuwa gera ishirini.* Shekeli ishirini, jumlisha na shekeli ishirini na tano, jumlisha na shekeli kumi na tano zitakuwa mina moja.*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.