Ezekieli 41:23
Ezekiel 41:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mahali patakatifu pa nje na Patakatifu Pa Patakatifu zilikuwa na milango miwili.
Ezekiel 41:23 in English
Ezekiel 41:23 · Berean Standard Bible
Both the outer sanctuary and the inner sanctuary had double doors,
Context
21Mahali patakatifu pa nje palikuwa na miimo ya mlango uliokuwa mraba na ule uliokuwa katika Patakatifu Pa Patakatifu ulikuwa unafanana na huo mwingine. 22Kulikuwa na madhabahu ya mbao kimo chake dhiraa tatu na ilikuwa dhiraa mbili mraba pande zote, tako lake na pande zake zilikuwa za mbao. Yule mtu akaniambia, “Hii ni meza ambayo iko mbele za Bwana.” 23Mahali patakatifu pa nje na Patakatifu Pa Patakatifu zilikuwa na milango miwili. 24Kila mlango ulikuwa na vipande viwili, vipande viwili vilivyoshikwa na bawaba vyenye kufunguka kwa kila mlango. 25Juu ya hiyo milango ya Patakatifu palinakshiwa makerubi na miti ya mitende kama yale yaliyonakshiwa kwenye kuta, na kulikuwa na ubao ulioningʼinia mbele ya baraza kwa nje.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.