Ezekieli 40:2
Ezekiel 40:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nikiwa katika maono ya Mungu alinichukua mpaka nchi ya Israeli, naye akaniweka kwenye mlima mrefu sana, ambako upande wa kusini kulikuwepo baadhi ya majengo ambayo yalionekana kama mji.
Ezekiel 40:2 in English
Ezekiel 40:2 · Berean Standard Bible
In visions of God He took me to the land of Israel and set me on a very high mountain, on whose southern slope was a structure that resembled a city.
Context
1Katika mwaka wa ishirini na tano wa uhamisho wetu, mwanzoni mwa huo mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kuanguka kwa mji, siku hiyo hiyo mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanipeleka huko. 2Nikiwa katika maono ya Mungu alinichukua mpaka nchi ya Israeli, naye akaniweka kwenye mlima mrefu sana, ambako upande wa kusini kulikuwepo baadhi ya majengo ambayo yalionekana kama mji. 3Akanipeleka huko, nami nikamwona mtu ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba. Alikuwa amesimama kwenye lango akiwa na kamba ya kitani na ufito wa kupimia mkononi mwake. 4Mtu huyo akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa macho yako na usikie kwa masikio yako nawe uzingatie kitu nitakachokuonyesha, kwa kuwa ndiyo sababu umeletwa hapa. Iambie nyumba ya Israeli kila kitu utakachoona.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.