Ezekieli 40:14
Ezekiel 40:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akapima pia ukumbi, urefu wa dhiraa ishirini* na lango linalofuatia hiyo nguzo kila upande wa huo ukumbi.
Ezekiel 40:14 in English
Ezekiel 40:14 · Berean Standard Bible
Next he measured the gateposts to be sixty cubits high.* The gateway extended around to the gatepost of the courtyard.
Context
12Mbele ya kila chumba cha kupumzikia kulikuwepo ukuta uliokuwa na kimo cha dhiraa moja* kwenda juu, navyo hivyo vyumba vilikuwa dhiraa sita mraba. 13Kisha akapima njia ya lango kuanzia juu ya ukuta wa nyuma wa chumba kimoja cha kupumzikia hadi juu ya ukuta wa nyuma wa chumba upande wa pili; kukawa na nafasi ya dhiraa ishirini na tano kuanzia lango la ukuta mmoja hadi lango la ukuta uliokuwa upande mwingine. 14Akapima pia ukumbi, urefu wa dhiraa ishirini* na lango linalofuatia hiyo nguzo kila upande wa huo ukumbi. 15Umbali kuanzia ingilio la njia ya lango hadi mwisho kabisa wa baraza yake ulikuwa dhiraa hamsini.* 16Kulikuwa na vidirisha kwenye hivyo vyumba vya walinzi na nguzo za hivyo vyumba zilikuwa kwenye mzunguko wa hilo lango, vivyo hivyo kulikuwa na madirisha yaliyozunguka kuelekeana na ua na juu ya kila nguzo kulikuwa na mapambo ya miti ya mitende.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.