Ezekieli 38:5
Ezekiel 38:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Uajemi, Kushi* na Putu watakuwa pamoja nao, wote wakiwa na ngao na kofia za chuma,
Ezekiel 38:5 in English
Ezekiel 38:5 · Berean Standard Bible
Persia, Cush,* and Put will accompany them, all with shields and helmets,
Context
3na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee Gogu, mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali. 4Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani, farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao. 5Uajemi, Kushi* na Putu watakuwa pamoja nao, wote wakiwa na ngao na kofia za chuma, 6pia Gomeri pamoja na vikosi vyake vyote, na Beth-Togarma kutoka kaskazini ya mbali pamoja na vikosi vyake vyote, mataifa mengi wakiwa pamoja nawe. 7“ ‘Jiandae, uwe tayari, wewe na makundi yako yote ya wajeuri yaliyokusanyika pamoja nawe, nawe waamrishe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.