Ezekieli 34:7
Ezekiel 34:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Kwa hiyo, ninyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana:
Ezekiel 34:7 in English
Ezekiel 34:7 · Berean Standard Bible
Therefore, you shepherds, hear the word of the LORD:
Context
5Hivyo walitawanyika kwa sababu hapakuwepo mchungaji, nao walipotawanyika, wakawa chakula cha wanyama wa mwitu wote. 6Kondoo wangu walitawanyika, wakatangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wa dunia yote bila kuwa na yeyote wa kuwaulizia wala wa kuwatafuta. 7“ ‘Kwa hiyo, ninyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana: 8Kwa hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, kwa sababu kondoo zangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama wote wa mwituni na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo zangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo zangu, 9kwa hiyo enyi wachungaji, sikieni neno la Bwana:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.