Ezekieli 31:9
Ezekiel 31:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Niliufanya kuwa mzuri ukiwa na matawi mengi, ulionewa wivu na miti yote ya Edeni katika bustani ya Mungu.
Ezekiel 31:9 in English
Ezekiel 31:9 · Berean Standard Bible
I made it beautiful with its many branches, the envy of all the trees of Eden, which were in the garden of God.’
Context
7Ulikuwa na fahari katika uzuri,
ukiwa na matawi yaliyotanda,
kwa kuwa mizizi yake ilikwenda chini
mpaka kwenye maji mengi. 8Mierezi katika bustani ya Mungu
haikuweza kushindana nao,
wala misunobari haikuweza
kulingana na vitawi vyake,
wala miaramoni
haikulinganishwa na matawi yake,
wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu
wa kulinganisha na uzuri wake. 9Niliufanya kuwa mzuri
ukiwa na matawi mengi,
ulionewa wivu na miti yote ya Edeni
katika bustani ya Mungu. 10“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake, 11niliutia mikononi mwa mtawala wa mataifa, ili yeye aushughulikie sawasawa na uovu wake. Nikaukatilia mbali,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.