Ezekieli 3:4
Ezekiel 3:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha akaniambia, “Mwanadamu, sasa nenda katika nyumba ya Israeli ukaseme nao maneno yangu.
Ezekiel 3:4 in English
Ezekiel 3:4 · Berean Standard Bible
Then He said to me, “Son of man, go now to the house of Israel and speak My words to them.
Context
2Ndipo nikafungua kinywa changu, naye akanilisha ule ukurasa wa kitabu. 3Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, kula ukurasa huu wa kitabu ninaokupa ujaze tumbo lako.” Kwa hiyo nikaula, ulikuwa mtamu kama asali kinywani mwangu. 4Kisha akaniambia, “Mwanadamu, sasa nenda katika nyumba ya Israeli ukaseme nao maneno yangu. 5Hukutumwa kwa taifa lenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli. 6Sikukutuma kwa mataifa mengi yenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu ambao maneno yao hutayaelewa. Hakika ningekutuma kwa watu hao, wangekusikiliza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.