Native Bible

Ezekiel 3:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mwishoni mwa hizo siku saba neno la Bwana likanijia kusema:

Ezekiel 3:16 in English

Ezekiel 3:16 · Berean Standard Bible

At the end of seven days the word of the LORD came to me, saying,

Context

14Ndipo Roho aliponiinua na kunipeleka mbali. Nikaenda nikiwa na uchungu na hasira moyoni mwangu, nao mkono wa Bwana ukiwa juu yangu. 15Nikafika kwa wale watu waliokuwa uhamishoni huko Tel-Abibu karibu na Mto Kebari. Nikakaa miongoni mwao kwa muda wa siku saba, nikiwa nimejawa na mshangao. 16Mwishoni mwa hizo siku saba neno la Bwana likanijia kusema: 17“Mwanadamu, nimekufanya uwe mlinzi wa nyumba ya Israeli, kwa hiyo sikia neno nisemalo, ukawape onyo litokalo kwangu. 18Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ na wewe usipomwonya mtu huyo au kumshauri aache njia zake mbaya ili kuokoa maisha yake, huyo mtu mwovu atakufa katika dhambi yake na damu yake nitaidai mkononi mwako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.