Ezekieli 25:2
Ezekiel 25:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Waamoni utabiri dhidi yao.
Ezekiel 25:2 in English
Ezekiel 25:2 · Berean Standard Bible
“Son of man, set your face against the Ammonites and prophesy against them.
Context
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Waamoni utabiri dhidi yao. 3Waambie, ‘Sikieni neno la Bwana Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulisema, “Aha!” juu ya mahali pangu patakatifu palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli ilipoangamizwa, na juu ya watu wa Yuda walipokwenda uhamishoni, 4kwa hiyo nitawatia mikononi mwa watu wa mashariki mkawe mali yao. Watapiga kambi zao katikati yenu na kufanya makazi miongoni mwenu, watakula matunda yenu na kunywa maziwa yenu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.