Ezekieli 21:12
Ezekiel 21:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Piga kelele na uomboleze, ee mwanadamu, kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu; u dhidi ya wakuu wote wa Israeli. Wametolewa wauawe kwa upanga pamoja na watu wangu. Kwa hiyo pigapiga kifua chako.
Ezekiel 21:12 in English
Ezekiel 21:12 · Berean Standard Bible
Cry out and wail, O son of man, for the sword is wielded against My people; it is against all the princes of Israel! They are tossed to the sword with My people; therefore strike your thigh.*
Context
10umenolewa kwa ajili ya mauaji,
umesuguliwa ili ungʼae
kama umeme wa radi!
“ ‘Je, tuifurahie fimbo ya utawala ya mwanangu Yuda? Upanga unaidharau kila fimbo ya namna hiyo. 11“ ‘Upanga umewekwa tayari ili kusuguliwa,
ili upate kushikwa mkononi,
umenolewa na kusuguliwa,
umewekwa tayari kwa mkono wa muuaji. 12Piga kelele na uomboleze, ee mwanadamu,
kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu;
u dhidi ya wakuu wote wa Israeli.
Wametolewa wauawe kwa upanga
pamoja na watu wangu.
Kwa hiyo pigapiga kifua chako. 13“ ‘Kwa maana upanga huu umejaribiwa na kuhakikishwa, itakuwaje basi fimbo ya ufalme ya Yuda inayoudharau kama haitakuwepo tena, bali itakuwa imeondolewa kabisa? asema Bwana Mwenyezi.’ 14“Hivyo basi, mwanadamu, tabiri
na ukapige makofi.
Upanga wako na upige mara mbili,
naam, hata mara tatu.
Ni upanga wa kuchinja,
upanga wa mauaji makuu,
ukiwashambulia kutoka kila upande.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.