Ezekieli 20:37
Ezekiel 20:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, nami nitawaleta katika mkataba wa Agano.
Ezekiel 20:37 in English
Ezekiel 20:37 · Berean Standard Bible
I will make you pass under the rod and will bring you into the bond of the covenant.
Context
35Nitawaleta katika jangwa la mataifa na huko nitatekeleza hukumu juu yenu uso kwa uso. 36Kama nilivyowahukumu baba zenu katika jangwa la nchi ya Misri, ndivyo nitakavyowahukumu ninyi, asema Bwana Mwenyezi. 37Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, nami nitawaleta katika mkataba wa Agano. 38Nitawaondoa miongoni mwenu wale wanaohalifu na wale wanaoasi dhidi yangu. Ingawa nitawatoa katika nchi wanazoishi, hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana. 39“ ‘Kwa habari zenu ninyi, ee nyumba ya Israeli, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.