Native Bible

Ezekiel 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo.

Ezekiel 2:3 in English

Ezekiel 2:3 · Berean Standard Bible

“Son of man,” He said to me, “I am sending you to the Israelites, to a rebellious nation that has rebelled against Me. To this very day they and their fathers have rebelled against Me.

Context

1Akaniambia, “Mwanadamu, simama kwa miguu yako nami nitasema nawe.” 2Alipokuwa akiongea nami, Roho akanijia na kunisimamisha wima, nikamsikia akisema nami. 3Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo. 4Watu ambao ninakutuma kwao ni wapotovu na wakaidi. Waambie, ‘Hivi ndivyo anavyosema Bwana Mwenyezi.’ 5Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.