Ezekieli 16:57
Ezekiel 16:57 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kabla uovu wako haujafunuliwa. Hata hivyo, sasa unadhihakiwa na binti za Edomu na jirani zake wote, na binti za Wafilisti, wale wote wanaokuzunguka wanakudharau.
Ezekiel 16:57 in English
Ezekiel 16:57 · Berean Standard Bible
before your wickedness was uncovered? Even so, you are now scorned by the daughters of Edom * and all those around her, and by the daughters of the Philistines—all those around you who despise you.
Context
55Nao dada zako, Sodoma na binti zake na Samaria na binti zake, watarudishwa kama vile walivyokuwa mwanzoni, nawe pamoja na binti zako mtarudishwa kama mlivyokuwa hapo awali. 56Hukuweza hata kumtaja dada yako Sodoma kwa sababu ya dharau yako katika siku za kiburi chako, 57kabla uovu wako haujafunuliwa. Hata hivyo, sasa unadhihakiwa na binti za Edomu na jirani zake wote, na binti za Wafilisti, wale wote wanaokuzunguka wanakudharau. 58Utachukua matokeo ya uasherati wako na matendo yako ya kuchukiza, asema Bwana. 59“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakushughulikia kama unavyostahili, kwa kuwa umedharau kiapo changu kwa kuvunja Agano.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.