Native Bible

Ezekiel 16:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“ ‘Ole! Ole wako! Asema Bwana Mwenyezi. Pamoja na maovu yako yote mengine,

Ezekiel 16:23 in English

Ezekiel 16:23 · Berean Standard Bible

Woe! Woe to you, declares the Lord GOD. And in addition to all your other wickedness,

Context

21Uliwachinja watoto wangu na kuwatoa kafara kwa sanamu. 22Katika matendo yako yote ya machukizo, pamoja na ukahaba wako hukukumbuka siku za ujana wako, wakati ulipokuwa uchi kabisa bila kitu chochote, ulipokuwa ukigaagaa kwenye damu yako. 23“ ‘Ole! Ole wako! Asema Bwana Mwenyezi. Pamoja na maovu yako yote mengine, 24Ukajijengea jukwaa na kujifanyia mahali pa fahari pa ibada za miungu kwenye kila uwanja wa mikutano. 25Katika kila mwanzo wa barabara ulijenga mahali pa fahari pa ibada za miungu na kuaibisha uzuri wako, ukiutoa mwili wako kwa kuzidisha uzinzi kwa kila apitaye.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.