Ezekieli 14:2
Ezekiel 14:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo neno la Bwana likanijia kusema:
Ezekiel 14:2 in English
Ezekiel 14:2 · Berean Standard Bible
And the word of the LORD came to me, saying,
Context
1Baadhi ya wazee wa Israeli walinijia na kuketi mbele yangu. 2Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 3“Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lolote? 4Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Wakati Mwisraeli yeyote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi Bwana nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.